Youth Partnership CountryWide (YPC)

Vijana Wapatiwa Mafunzo ya Ujasiriamali Kupitia YPC

Mkuu wa wilaya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA amekemea tabia ya wanajamii kuwaita vijana kuwa ni bomu ambalo linasubiriwa kulipuka muda wowte bila kutafuta mbinu mwafaka za kuwaondoa katika ukosefu wa kazi kwa kuwapatia mafunzo na mtaji wa kuanzisha biashara na miradi ya kilimo na ufugaji.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kibaha, BIBI HALIMA KIHEMBA amesema juhudi ambazo zinaonyeshwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama ambavyo YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE ambalo limewapatia vijana mafunzo kuhusiana masuala ya ujasiriamali ambapo kutasaidia kuwafanya vijana kubadilisha mtazamo kutoka kwa uliopo sasa wa kuwa vijana ni bomu linalongojea kulipuka mpaka kuwa wazalishaji wakuu ambao nguvu kazi yao itakuwa tegemeo kwa Taifa.

Hayo ameyazungumza katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa Kibaha ambvayo yanmefadhiliwa kwa asilimia kubwa na shirika la kazi ulimwenguni -ILO-, Na amekataa kukubaliana na dhana ya kuwa vijana ni wavivu wakati hakuna mazingira rafiki yanayoandaliwa kumsaidia kijana anapotaka kufanya mradi wowote ikiwaa pamoja na ngazi ya halmashauri kutoa kipaumbele kwa kada hii ambayo ndio wengi kupita raia wengine nchi na inakadiriwa kuwa kundi la vijana nia asilimia 65 ya Watanzania wote. BIBI. KIHEMBA amebainisha kutokana na kundi hilo muhimu katika jamii kuachwa bila kupewa usaidizi wowote tumeshuhudia likiijingiza katika vitendo vya uvinjifu wa amani, kwa kukubali kutumika na watu wasioitakia mema nchi yetu kufanya vurugu kwa visingizio vya kidini kama ambavyo imeshuhudiwa hivi karibuni katika matukio ambayo yametokea Zanzibar, Dar Es Saalam na maeneo ya mkoa wa Pwani ya Rufiji, na Bagamoyo.

Afisa mipango wa shirika lisilo la Kiserikali la YPC lenye maskani yake mjini Kibaha mkoa wa Pwani. BW. SAMUEL STANLEY amesema katika awamu ya pili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wamenuia kuchukua vijana 400, ambo watapatiwa mafunzo ya uchumi na ujasiriamali. BW. STANLEY amebainisha mpaka sasa wameshafanikiwa kuzalisha vijana kadhaa ambao wana elimu ya kutosha ya ujasiriamali, ambapo mpka sasa wameshafanya maonyesho ya bidhaa ambazo wanazalisha ikiwa ni mchango ambao umetolewa katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo ambayo ilikuwa inajulikana kama mpango wa kazi nje nje mpaka kukamilika kwa mafunzo hayo takribani shilingi milioni 36 zinatarajia kutumika katika kipindi cha miezi sita ijayo. END.